Skip to main content

Mapendekezo ya afya ya umma ya kukomesha COVID-19 (Swahili)

Mapendekezo ya afya ya umma ya kukomesha COVID-19

Public Health Recommendations to Stop COVID-19 in Swahili

Tafadhali tembelea tovuti ya Idara ya Afya katika Jimbo la Washington ili kupata taarifa iliyotafsiriwa kuhusu COVID-19. Unaweza kutumia menyu kunjuzi ya lugha ili kupata tafsiri zote walizo nazo.

Chukua hatua hizi ili kusaidia kudhibiti maenezi ya virusi vya corona na kuweka kila mmoja salama.

Kinga bora ni kupata chanjo. Watu waliopewa chanjo kamili sasa wanaweza kufanya vitu vingi zaidi kwa njia salama na wanasaidia kupunguza ugonjwa wa COVID-19 katika jamii.

Kuvalia maski/barakoa katika mazingira yenye hatari kubwa ya kupata maambukizi (kama vile maeneo yenye watu wengi) inasaidia kulinda kila mtu. Ni muhimu sana kuwalinda watu ambao hawawezi kupata kinga kamili kutoka kwa chanjo, kama vile watoto wadogo na watu walio na hali za kimatibabu ambao wanauwezo mdogo wa kupambana na virusi.

Nenda upimwe (Bogga waa Engiriis kaliya) ikiwa una dalili za ugonjwa wa COVID-19 au umekuwa karibu na mtu ambaye amepatikana na virusi vya COVID-19.

Ikiwa utapatikana na COVID-19 au uko katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo, kupata matibabu ya COVID-19 mapema (maelezo kwa Kiingereza tu) kunaweza kusaidia kujikinga na ugonjwa mbaya na kulazwa hospitalini. Uliza mtoaji wako wa huduma ya afya kuona ikiwa matibabu yanapendekezwa kwako.

Weka shughuli ziwe na watu wachache na zifanyike nje ya majengo ikiwa watu ambao hawajachanjwa watashiriki. Virusi huenea kwa urahisi ndani ya majengo, kwa hivyo biashara na mashirika yanaweza kupunguza virusi hewani kwa kuwa na mtiririko mzuri wa hewa ndani ya majengo na kutumia vichujio vya hewa (tovuti ni kwa kiingereza).


Usaidizi unapatikana

Iwapo unahitaji huduma za ukalimani katika lugha nyingine au usaidizi mtandaoni, piga simu kwa Nambari ya Simu ya katika Jimbo la Washington. Hatuulizi kuhusu hali yako ya uhamiaji. Mtu yeyote atapokea usaidizi usaidizi, licha ya hali yao.

Ili kuomba usaidizi:

  1. 1-800-525-0127
  2. Ujumbe utachezwa. Msubiri mwendeshaji wa kituo cha simu ili akujibu.
  3. Sema lugha unayotaka.
  4. Mwendeshaji wa kituo cha simu atapiga simu kwa huduma ya ukalimani. Usikate simu. Kaa kwenye simu hadi utakapounganishwa na mkalimani.

Mwongozo wa COVID-19


Mkusanyiko wa taswira za data kama vile chati za pai Na grafu

Uwe tayari kusaidiana. Umoja wa jamii utatuimarisha katika wakati huu mgumu.


Link/share our site at www.kingcounty.gov/covid/swahili

expand_less