Skip to main content
King County logo

Kwa mtu yeyote ambaye hajachanjwa kikamilifu/hajapata chanjo kamili,  Agizo la Idara ya Afya ya jimbo (kwa kiingereza) pia inaendelea kutumika/kufanya kazi:Watu ambao hawajachanjwa kikamilifu/hawajapata chanjo kamili wanahitajika "kuvalia vifaa vya kufunika uso/maski/barakoa katika mazingira yoyote ya ndani ya majengo yanayotumika na umma, au wakiwa nje ya majengo na hawawezi kuzingatia umbali wa futi sita na watu wengine."

Kila mmoja anapaswa pia kuvalia maski/barakoa vizuri katika:

  • Vituo vya marekebisho;
  • Makao ya watu wasiokuwa na makazi;
  • Shule na sehemu za utunzaji wa watoto;
  • Usafiri wa umma, na;
  • Maeneo ya utunzaji wa afya kama vile afisi ya daktari, utunzaji wa muda mrefu, na hospitali

Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) hivi karibuni vilisasisha mwongozo wake kuruhusu watu waliopewa chanjo kamili kuwacha kuvalia maski/barakoa katika maeneo mengi. Mkurugenzi wa CDC Rochelle Walensky na Idara ya Afya ya Jimbo la Washington baadaye walifafanua kwamba jukumu la kuvalia maski/barakoa ndani ya majengo inapaswa kuhusishwa na viwango vya COVID-19 mtaani na viwango vya usambazaji wa chanjo.

Ikiwa una maswali kuhusu kile kinachoendelea katika Kaunti ya King, tafadhali piga simu kwa kituo cha simu cha COVID-19 cha Kaunti ya King kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku. Jumatatu – Ijumaa kwa nambari 206‑477‑3977. Msaada wa lugha unapatikana.