Skip to main content
King County logo

Agizo la Kaunti ya King ya kuvalia Maski/Barakoa ndani ya majengo itakamilika tarehe 11 Machi, 2022

Hiyo ina maana gani kuanzia tarehe 12 Machi?

Maski/Barakoa hazitahitajika tena katika maeneo mengi ya ndani ya majengo ya umma:

  • Shule, vituo vya kuwatunza watoto na maktaba
  • Mikahawa na Baa
  • Nyumba za ibada/kuabudu
  • Maeneo ya kufanyia mazoezi, vituo vya burudani na maeneo ya ndani ya kushiriki riadha
  • Maduka ya kuuzia vyakula, Biashara na maduka ya rejareja

Maski/Barakoa bado zinahitajika:

  • Katika maeneo ya kutoa huduma za afya na matibabu,ikijumuisha hospitali, vituo vya kuwatibu watu wasiolazwa,vituo vya kutibu meno na maduka ya dawa
  • Maeneo ya utunzaji wa muda mrefu
  • Vituo vya kurekebisha tabia

Biashara za kibinafsi,mashirika, shule na maeneo ya kuwatunza watoto bado yanaweza chagua kutekeleza mahitaji yao kuhusu Maski/Barakoa. Tafadhali heshimu maamuzi ya watu ya kuendelea kuvaa maski/barakoa.

Chukua hatua hizi ili kusaidia kudhibiti maenezi ya virusi vya corona na kuweka kila mmoja salama.

Kinga bora ni kupata chanjo. Watu waliopewa chanjo kamili sasa wanaweza kufanya vitu vingi zaidi kwa njia salama na wanasaidia kupunguza ugonjwa wa COVID-19 katika jamii.

Kuvalia maski/barakoa katika mazingira yenye hatari kubwa ya kupata maambukizi (kama vile maeneo yenye watu wengi) inasaidia kulinda kila mtu. Ni muhimu sana kuwalinda watu ambao hawawezi kupata kinga kamili kutoka kwa chanjo, kama vile watoto wadogo na watu walio na hali za kimatibabu ambao wanauwezo mdogo wa kupambana na virusi.

Nenda upimwe ikiwa una dalili za ugonjwa wa COVID-19 au umekuwa karibu na mtu ambaye amepatikana na virusi vya COVID-19.

Ikiwa utapatikana na COVID-19 au uko katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo, kupata matibabu ya COVID-19 mapema (maelezo kwa Kiingereza tu) kunaweza kusaidia kujikinga na ugonjwa mbaya na kulazwa hospitalini. Uliza mtoaji wako wa huduma ya afya kuona ikiwa matibabu yanapendekezwa kwako.

Weka shughuli ziwe na watu wachache na zifanyike nje ya majengo ikiwa watu ambao hawajachanjwa watashiriki. Virusi huenea kwa urahisi ndani ya majengo, kwa hivyo biashara na mashirika yanaweza kupunguza virusi hewani kwa kuwa na mtiririko mzuri wa hewa ndani ya majengo na kutumia vichujio vya hewa (tovuti ni kwa kiingereza).


Mwongozo wa COVID-19

Uwe tayari kusaidiana. Umoja wa jamii utatuimarisha katika wakati huu mgumu.


Link/share our site at www.kingcounty.gov/covid/swahili